Hujjatul Islam Sayyid Muhammad Hassan Abu Turabi Fard amesema hayo leo mbele ya hadhara ya waumini waliohudhuria ibada ya kimaanawi na kisiasa ya Swala ya Ijumaa mjini Tehran ambapo ameashiria matukio ya Palestina na mashambulizi ya kinyama ya utawala wa Kizayuni katika mji wa Rafah ulioko kusini mwa Ukanda wa Gaza na kuongeza kuwa, hii leo hii Rafah inayodhulumiwa na yenye nguvu imegeuka na kuwa ndio mwisho wa Israel licha ya kuwa na zana na silaha ambazo Marekani imetoa kwa utawala huo ghasibu na taasisi za kimataifa zimeziunga mkono hilo.
Sayyid Abu Turabi Fard amebainisha kuwa, licha ya hayo yote, lakini Gaza bado imesimama kidete.
Khatibu wa Swala ya Ijumaa ya leo mjini Tehran amesema pia kuwa, jinai, mikono ya Wazayuni iliyotapakaa damu, Magharibi na Marekani, imeondoa pazia la ujinga na mghafala machoni pa walimwengu na kuamsha dhamiri.
Kadhalika amesema, mauaji hayo hayasababishi watu wa Gaza kuyahama makazi yao na wala hayafuti jiografia ya kisiasa ya dunia na kwamba, hamasa ya damu ya Gaza lazima ishinde, na hiyo ndiyo Gaza, na ujenzi wake upya na nchi za Kiislamu ni muhimu.
342/